User:Mudbringer/Sandbox/Parallel002

Kisa cha punda wa dobi — The Story of the Washerman's Donkey edit

source

Aliondokea kima akafanya urafiki na papa. Pana mti mkubwa, jina lake mkuyu, umeota katika kilindi, matawi yake nussu yako mjini, na nussu yako baharini. Yule kima kulla siku kwenda akila kuyu, na yule rafiki yake papa huwapo chini ya mti. Humwambia, utupie nami rafiki yangu vyakula; humtupia siku nyingi na miezi mingi. There was once a monkey which made friends with a shark. There was a great tree, of the sort called mkuyu, which grew near the deep water; half its branches were over the town and half over the sea. The monkey used to go every day and eat the kuyu fruit, and his friend the shark was there under the tree. He used to say, "Throw me some food, my friend;" and he used to throw to him, many days and many months.
Hatta siku hiyo papa akamwambia kima, fathili zako nyingi, nataka twende kwetu nikakulipe fathili. Kima akamjibu, ntakwendaje, nasi hatuingii majini, nyama wa barra. Akamwambia, ntakuchukua, tone la maji lisikupate. Akamwambia, twende. Till one day the shark said to the monkey, "You have done me many kindnesses, I should like for us to go to my home, that I may repay you for your kindness." The monkey answered him, "How shall I go? We don't go into the water, we beasts of the land." And he said, "I will carry you; not a drop of water shall get to you." And he said, "Let us go."
Wakaenda zao hatta nussu ya njia. Papa akamwambia, rafiki yangu weye, ntakwambia kweli. Akamwambia, niambie. Akamwambia, huko kwetu tunakokwenda, Sultani wetu hawezi sana, na dawa tumeambiwa ni moyo wa kima. Kima akamjibu, hukufanya vema usiniambie kulekule. Papa akamwuliza, ginsi gani? They went half the way. And the shark said, "You are my friend, I will tell you the truth." He said, "Tell me." He said, "There, at home, where we are going, our Sultan is very ill, and we have been told that the medicine for him is a monkey's heart." The monkey replied to him, "You did not do well not to tell me there on the spot." The shark said, "How so?"
Akafikiri kima akaona, nimekwisha kufa; sasa ntanena uwongo, labuda utanifaa. The monkey considered, and felt, "My life is gone already; now I will tell him a lie, perhaps that may serve me."
Papa akamwuliza, umenyamaza huneni? Akamwambia, sina la kunena, kwani usiniambie kulekule, nikapata kuchukua moyo wangu. Papa akamwuliza, hapa, kunao moyo wako? The shark asked him, "You have become silent; don't you speak?" He said, "I have nothing to say, because your not telling me there on the spot, and I might have brought my heart." The shark asked, "Have you your heart here?"
Huna khabari yetu? Sisi tukitembea mioyo yetu huacha mitini tukatembea viwiliwili tu, wallakini hutanisadiki, utaniambia nimeogopa, sasa twende zetu hatta huko kwenu, ukanichinje kama utauona moyo wangu. "Don't you know about us? When we go out we leave our hearts in the trees, and we go about with only our bodies; but you won't believe me, you will tell me I am afraid; let us go on now to your home there, and kill me if you find my heart."
Papa akasadiki, akamwambia kima, turudi sasa, ukatwae moyo wako. Kima akamwambia, sikubali, ela twende kwenu. Akamwambia, turudi kwanza ukatwae moyo wako, tupate kuenenda. The shark believed it, and said to the monkey, "Let us go back now, and you get your heart." The monkey said, "I don't agree to that, but let us go to your place." And he said, "Let us go back first and take your heart, that we may go on."
Kima akawaza - ni heri kumfuata hatta mtini, akili nnayo mwenyewe nikiisha fika. Wakaenda wakarudi hatta mtini, akapanda juu yule kima akamwambia, ningoje hapa, papa, naenda twaa moyo wangu, tupate kwenda zetu. The monkey considered - I had better consent to him as far as to the tree, I know what to do when I have got there. They went and returned to the tree, and the monkey clunbed up, and said, "Wait for me here, shark, I am going to get my heart, that we may be off."
Akapanda mtini akakaa kitako kimya. Papa akamwita. Akanyamaza. Akamwita tena. Akamwambia, twende zetu. Kima akamjibu, twende wapi? Akamwambia, twende kwetu. Akamwambia, una wazimo? Papa akamwuliza, ginsi gani? Kima akamwambia, umenifanya punda wa dobi? Papa akamwuliza kima, ginsi gani punda wa dobi? Akamwambia, Ndiye hana moyo, wala hana mashikio. Papa akamwuliza, ginsi gani kisa cha punda wa dobi? Nambie, rafiki yangu, nipate kujua maana. He climbed into the tree and sat down quite still. The shark called him. He held his tongue. He called him again and said, "Let us be going." The monkey answered him, "Let us go where?" He said, "Let us go to our home." He said, "Are you mad?" The shark said, "How so?" The monkey said to him, "Do you take me for a washerman's donkey?" The shark asked the monkey, "What about a washerman's donkey?" He said, "That's what has neither heart nor ears. "The shark said, "What is the story of the washerman's donkey? Tell me, my friend, that I may know what it means."
Akamwambia, Dobi alikuwa na punda wake, akimpenda sana mwenyewe. Akakimbia punda akaingia mwituni siku nyingi, hatta akamsahao mwenyewe dobi. Akanenepa sana kule mwituni. And he said, "A washerman had a donkey, and its owner was very fond of it. And the donkey ran away, and went into the forest many days, till its owner the washerman forgot it. And it got very fat there in the forest.
Akapita sungura, akamwona yule punda, mate yakamtoka, akanena, nyama imenona hii. Akaenda akamwambia simba. Na simba atoka ugonjwani, amekonda sana. Sungura akamwambia, ntakuleta nyama kesho, tuje tule. Akamwambia, vema. And the hare went by and saw the donkey, and foam coming from its mouth, and he said, 'This beast is fat.' And he went and told the lion. Now the lion was recovering from an illness; he was very weakly. The hare said to him, 'I will bring you some meat to-morrow, that we may come and eat.' The lion said, 'Very good.'
Sungura akaondoka, akaenda mwituni, akamwona punda, na yule punda mke. Akamwambia, nimetumwa kuja kukuposa. Na nani? akamwuliza. Akamwambia, na simba. Akakubali, akafurahi sana punda. Akamwambia, Twende zetu, bass. "The hare arose and went into the forest, and found the donkey; now that donkey was a she. And he said to her, 'I am sent to come and ask you in marriage.' 'By whom?' she asked. And he said, 'By the lion.' And the donkey consented, and was very glad. And she said, 'Let us go, that will do.'
Wakaenda zao, hatta wakafika kwa simba. Akawakaribisha simba. Wakakaa kitako. Sungura akamkonyeza simba, akamwambia, nyama yako hiyo imekwisha kuja, nami naondoka. Akamwambia punda, nnakwenda chooni mimi, zumgumzeni hapo na mumeo. "And they went, till they arrived at the lion's. And the lion invited them in, and they sat down.? The hare gave the lion a sign with his eyebrow, telling him, 'This is your meat, it has come with me abeady; I am going out,' And he said to the donkey, 'I am going on private business, converse here with your husband.'
Simba akamrukia, wakapigana, akapigwa sana simba kwa mateke, naye akampiga makucha mengi. Akaangusha simba akakimbia punda, akaenda zake mwituni. Akaja sungura, akamwambia, Je! simba, umempata? Akamwambia, sikumpata, amenipiga kwa mateke amekwenda zake, na mimi nimemtia madonda mengi, sababu sina nguvu. Sungura akamwambia simba, tulia we. "The lion sprang upon her, and they fought: the lion was kicked very hard, and he struck hard with his claws. And the donkey threw the lion down and ran away, and went off into the forest. The hare came and said, 'Hullo! lion, have you got it?' He said, 'I have not got it; she kicked me and went off, though I have made her many sore places, because I am not strong.' The hare said to the lion, 'Don't put yourself out of the way.'
Wakakaa siku nyingi, hatta punda akapona madonda yale, na simba akapata nguvu sana. Akaenda sungura kwa simba, akamwambia, waonaje sasa, nikuletee nyama yako? Akamwambia, kaniletea ntaikata vipande viwili. "They stayed many days, till the donkey was well of her wounds, and the lion had got very strong. And the hare went to the lion and said, 'What do you think now, shall I bring you your meat?' He said, 'Bring it me, I will tear it into two pieces.'
Akaenda sungura mwituni. Punda akamkaribisha sungura, akamwuliza khabari. Akamwambia, na mchumba wako anakwita. Punda akamwambia, siku ile umenipeleka, amenipiga sana kwa makucha, naogopa sasa. Akamwambia, hapana neno yalio ndio mazumgumzo ya simba. Akamwambia, twende zetu, bass. "The hare went into the forest; the donkey welcomed the hare, and asked the news. He said, 'You are invited by your lover.' The donkey said, 'That day you took me, he scratched me very much, and now I am afraid.' And he said, 'That is nothing, it is only the lion's way of conversing.' She said, 'Let us go, then.'
Wakaenda hatta wakafika. Simba alipomwona tu, akamrukia akamkata vipande viwili. "They went till they arrived. The lion, when he had only caught sight of her, sprang upon her and tore her in two pieces.
Hatta sungura alipokuja, akamwambia, chukua nyama hiyo ukaoke, wallakini sitaki kitu mimi, ela moyo na mashikio ya punda. Sungura akamwambia, marahaba. Akaenda akaoka nyama mahala mbali, simba hamwoni. Akatwaa moyo ule na mashikio akala yeye sungura, hatta akashiba. Na nyama ngine akaziweka. "When the hare came, he said to him, 'Take this meat and roast it; but myself I want nothing except the donkey's heart and ears.' The hare said, 'Thanks.' And he went and roasted the meat in a place apart, where the lion did not see him. And the hare took the heart and ears, and went on eating himself, till he had had enough. And the rest of the meat he put away.
Akaja simba, akamwambia, niletee moyo na mashikio. Akamwambia, yako wapi? Simba akamwuliza, kwa nini? Akamwambia, huyu punda wa dobi, huna khabari? Akamwambia, ginsi gani kutoa kuwa na moyo na mashikio? Akamwambia, wewe simba mtu mzima hayakuelei? Kama ana moyo huyu na mashikio, angalikuja tena hapa? Kwani marra ya kwanza amekuja akaona atakuuawa, akakimbia, marra ya pili amekuja tena, bassi kama ana moyo angalikuja? Simba akamwambia, kweli maneno yako. "And the lion came and said, 'Bring me the heart and ears.' He said, 'Where are they?' The lion asked him, 'What does this mean?' He said, 'This was a washerman's donkey, did not you know?' And he said, 'What about there being no heart and ears?' He said, 'You lion, a grown-up person, and is it not clear to you? If this animal had had heart and ears, would it have come here a second time? For the first time it came, it saw it would be killed, and ran away; and yet i t came again the second time. Now, if it had any heart, would it have come?' The lion said, 'There is truth in what you say.'"
Bassi kima akamwambia papa, nawe wataka unifanye mimi punda wa dobi, shika njia wende zako kwenu, mimi hunipati tena, na urafiki wetu umekwisha. Kua heri. So the monkey said to the shark, "And you want to make a washerman's donkey of me. Take your way and be off home, you are not going to get me again, and our friendship is ended. Good-bye."